[index]
ibs
1 Corinthiens 13
1 Hata
kama nikinena lugha za watu na hata za malaika, lakini kama sina upendo mimi nimekuwa
tu kama sauti ya debe tupu au kengele.
2 Tena, naweza kuwa na kipaji cha
kutangaza ujumbe wa Mungu, nikafahamu siri zote na kujua kila kitu; naweza kuwa
na imani yote hata nikaweza kuihamisha milima, lakini kama sina upendo mimi si
kitu.
3 Nikitoa mali yangu yote na kuwapa maskini, na tena nikiutoa mwili
wangu uchomwe, kama sina upendo hiyo hainifai chochote.
4 Mwenye upendo
huvumilia, hufadhili; mwenye upendo hana wivu, hajidai, wala hajivuni.
5
Mwenye upendo hakosi adabu, hatafuti faida yake binafsi, wala hana wepesi wa hasira;
haweki kumbukumbu ya mabaya,
6 hafurahii uovu, bali hufurahia ukweli.
7
Mwenye upendo huvumilia yote, huamini yote, na hustahimili yote.
8 Upendo
hauna kikomo kamwe. Kama kuna vipaji vya kutangaza ujumbe wa Mungu, hivyo vitatoweka
siku moja; kama ni vipaji vya kusema lugha ngeni, vitakoma; kama kuna elimu, nayo
itapita.
9 Maana ujuzi wetu si kamili, na kipaji chetu cha kutangaza
neno la Mungu si kamili.
10 Lakini kile kilicho kikamilifu kitakapofika,
vyote visivyo vikamilifu vitatoweka.
11 Nilipokuwa mtoto mchanga nilisema
kitoto, nilifahamu kitoto, nilifikiri kitoto. Lakini sasa, maadam mimi ni mtu
mzima, mambo ya kitoto nimeyaacha.
12 Tunachoona sasa ni kama tu sura
hafifu katika kioo, lakini hapo baadaye tutaona uso kwa uso. Sasa ninajua kiasi
fulani tu, lakini hapo baadaye nitajua yote kikamilifu, kama vile Mungu anavyonijua
mimi.
13 Sasa yanadumu haya matatu: imani, tumaini na upendo; lakini
lililo kuu kupita yote ni upendo.
[index]